VIFAA VYA KUFUNDISHIA

Report
Nini maana ya vifaa vya kufundishia?



Ni kitu chochote kinachotumiwa na mwalimu
/mwanafunzi kwa ajili ya kushajihisha
usomeshaji na kujifunza.
Vipo vifaa ambavyo mwalimu ndio anatumia
zaidi (ubao, projector, nk)
Vipo ambavyo mwalimu na mwanafunzi
wanatumia kwa pamoja (vitabu vya kiada)

Unafikiri sifa gani zinahitajika kwa Kifaa cha
kufundishia kilichobora na kitakachopelekea
lengo la kujifunza kufikiwa?

Angalia kwa makini vifaa vifuatavyo kisha toa
maoni yako.
KIELEZI
NOMINO
KITENZI
AINA ZA
MANENO
KIVUMISHI
KIWAKILISHI
Aina za
sentensi
Sentensi
sahili
Sentensi
ambatano
Sentensi
shurtia
Sentensi
changam
ano


FISI AADHIBIWA
Hapo zamani katika mbuga ya Rijeni wanyama wadogo walikutana kwa siri kujadili uovu wa Fisi. Walikutana kwa siri kwa sababu walijua
wanyama kama Simba, Chui na Fisi walikuwa na hamu kubwa ya kuwashambulia na kuwala. Swala alikuwa kiongozi wa mkutano na
akawaambia wenzake, “Jamani, uonevu umezidi. Juma lililopita watoto wawili wa Kongoni waliliwa na Chui, tena Chui alisema hakushiba.
Alitaka sana amshike Kongoni amle, lakini Kongoni aliwahi kukimbia. Juzi mwanangu Ameliwa na Fisi. Nilimpiga teke jichoni lakini
akataka kunitafuna, nikakimbia, sasa tufanyeje?”


Basi wanyama walijadili kwa uchungu na kwa muda mrefu. Wote walitaka sana Chui na Fisi wauawe haraka. Tatizo lao kubwa lilikuwa
jinsi ya kuwauwa. Wengine walishauri waovu wale wategewe mitego ya kamba baadaye wapofuliwe. Hata hivyo ilionekana ni hatari bado.
Hatimae sungura akatikisa masikio yake na kusema, “Kuwauwa niachieni mimi. Nipeni siku saba nitawaeleza na kuwaonesha
nitakachofanya.” Basi mkutano ukafungwa na kumkubalia Sungura afanye kazi hiyo. Usiku ulipoingia Sungura alikoka moto nje ya
nyumba yake. Moto ulipokolea vizuri akatia jiwe moja ndani ya ule moto. Jiwe hilo lilikuwa na ukubwa wa mpira wa tenisi. Sungura
akaongeza kuni mekoni halafu akaenda kumtafuta Fisi pangoni mwake.


Sungura alipofika mlangoni mwa pango akasema, “hodi kwa mzee Fisi!” Fisi alifurahi moyoni, kwa sababu alijua ile sauti ya Sungura na
alijua kuwa Sungura angeweza kuwa chakula chake. Fisi hakujibu haraka. Kwa hiyo Sungura akasogea mlangoni na kubisha tena hodi.
Hapo ndipo Sungura alipojikuta makuchani mwa Fisi! Sungura akaona kifo waziwazi .Sungura akamwambia “rafiki yangu mzee Fisi vipi
leo? Nakuletea habari nzuri halafu unanikamata!” Fisi akasema mimi nina njaa ya siku nne halafu uniletee habari nzuri gani? “Wewe ni
rafiki yangu” Sungura akampoza , “hata kama utanila hutashiba. Mimi nimekuja nikukaribishe kwangu. Huko nyama ni tele.”


Fisi alifurahi na kucheka huku akimwachia Sungura . “Haya ongoza njia. Tena uongeze mwendo, sio ule mwendo wako wa sisimizi”.
Sungura na Fisi walifika kwa Sungura huku mate yanamtoka Fisi mdomoni kwa hamu ya nyama. Hapo Sungura akapanga vitimbi vyake
akasema, “mzee fisi nyama zipo nyingi lakini hizi ni nyama za tambiko. Kwa desturi za kwetu mnofu wa kwanza nitakulisha mimi
mwenyewe, mradi ulale chali na ufumbe macho”. Baada ya hapo nyama nyengine utakula kwa mikono yako.” Kabla Sungura hajamaliza
Fisi alikwisha lala chali, na kufungua mdomo na pia kufumba macho.


Sungura alicheka kimoyomoyo akatwaa kibanio, akabana lile jiwe la moto na kulitumbukiza mdomoni mwa Fisi. Kwa kuwa Fisi alikuwa
amejiandaa kumeza nyama , alilimeza jiwe haraka sana. Looo! Fisi aliungua koo, kifua na tumbo. Fisi alibiringika akilia sana na kujitupa
huku na huko hadi akakata roho.


(Kutoka, Kiswahili 2 - Kidato cha Pili, Taasisi ya Elimu, Oxford University Press, Dar Es Salaam, 1996, uk 5-6.)







Vifahamike
Visomeke
Visikike
Vionekane (viwe vikubwa vya kutosha)
Viwasilishe dhana iliyokusudiwa
Viendane na maadili ya jamii
Vilingane na viwango vya wanafunzi






Visiwe na athari kwa wanafunzi
Visimjenge khofu mwanafunzi
(kutokueleweka,nk)
Vimsaidie mwanafunzi
kujiamini,vimhamasishe
Visiwe na tafsiri nyingi/dhana nyingi kwa
wakati mmoja
Vizingatie tofauti ya wanafunzi katika
ufahamu/ugumu
Vichorwe vizuri vivutie (attractive)







Picha za vitu halisi
Vitu halisi
Michoro (drawings)
Vivuli vya mazungumzo au habari
Redio na vinasa sauti
Ramani
Chati na vielelezo






Kadi zenye malekezo
Vitabu vya kiada
Ubao na chaki
Vipande vya habari vilivyotayarishwa na
mwalimu, kutoka magazetini, vitabuni,nk
Projecta
computer






Kurahisisha ufahamu kwa wanafunzi
Kuwachangamsha wanafunzi
Kuwashirikisha wanafunzi ,kutumia akili zao
kwa kuzalisha mawazo yatokanayo na vifaa
vinavyotumika
Kuhifadhi muda
Vinapelekea Kumbukumbu ya muda mrefu
Vinasaidia maneno (support verbal
instructions)

Vinapelekea kuifanya dhana kuonekana
(verbal idea to be concrete)

Ref. Mbumda F. (1996)Mbinu za Kufundisha

Tomlison Brian (2004)Material development
lugha ya Kiswahili
in language teaching

similar documents